Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, mwanahabari Fadi Boudia ameandika kwenye jukwaa la X kwamba kwa mara ya kwanza Iran imetangaza rasmi kufikiwa kwa rasimu ya mwisho ya makubaliano kati yake na Marekani, huku Ijumaa ikitajwa kuwa siku iliyopangwa kwa ajili ya kutiwa saini kwa makubaliano hayo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, macho sasa yanaelekezwa kwenye tamko rasmi litakalotolewa na pande husika, ambalo linatarajiwa kufafanua msimamo na maelezo ya kina kuhusu makubaliano hayo.
Fadi Boudia ameongeza kuwa ikiwa Israel itazingatia usitishaji wa mapigano nchini Lebanon, hatua hiyo itatazamwa kama matokeo ya ustahimilivu mkubwa wa Harakati za Muqawama katika kukabiliana na Israel, pamoja na msimamo wa Iran wa kusisitiza kwamba suala la
Lebanon lijumuishwe katika makubaliano yoyote na lisitenganishwe na muktadha wa mapambano ya eneo hilo, kwa kuzingatia kile kinachoitwa "umoja wa medani za mapambano."
Hata hivyo, madai hayo yanasubiri kuthibitishwa kupitia taarifa rasmi kutoka kwa mamlaka zinazohusika kuhusu maudhui ya makubaliano na utekelezaji wake.
Your Comment